Michezo

Mkwasa, amtambulisha Ofisa Habari mpya Yanga

Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa leo amemtambulisha Dissmas Ten kuwa Ofisa Habari mpya na  wa nne wa klabu hiyo tangu mwaka 2010, akirithi nafasi ya Jerry Muro anayemaliza mkataba wake.

Dissmas Ten (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari, Charles Boniface Mkwasa (kulia) akimsikiliza. Kushoto ni Godlisten Anderson ‘Chicharito’

Louis Sendeu alikuwa Ofisa Habari wa kwanza wa Yanga mwaka 2010 chini ya Mwenyekiti, Wakili Imani Mahugila Madega aliyedumu hadi uongozi wa Mwenyekiti Wakili Lloyd Baharagu Nchunga kisha kutolewa mara baada ya kuingia kwa uongozi mpya wa Mwenyekiti Yussuf Manji.

Ambapo kijiti cha nafasi hiyo kilichukuliwa na Baraka Kizuguto aliyekaimu kwa muda kisha kuchukuliwa na Muro, lakini kabla ya kumaliza muda wake ndipo akakutana na rungu la adhabu kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ kwa makosa ya kimaadili.

Adhabu ya Muro imemalizika huku mkataba wake na klabu hiyo ukiwa nao umefikia mwisho na hivyo nafasi yake ikichukuliwa na siku chache baada ya kumaliza adhabu yake, Muro anaondolewa kazini na nafasi yake ikichukuliwa na Dissmas Ten .

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents