Michezo

Video: RC Makonda aeleza kwanini kijana aliyemkumbatia Rooney aliachiwa

Mechi kati ya Everton na Gor Mahia iliyochezwa Uwanja wa Taifa Alhamisi hii imeacha matukio mengi ya kihistoria katika soka nchini Tanzania. Mchezo huo ulimalizika kwa vijana hao wa Donald Koeman kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Kijana akimkumbatia, Wayne Rooney

Moja ya tukio kubwa ambalo lilijitokeza katika mchezo huo ni lile la shabiki kuingia uwanjani katikati ya mchezo na kwenda kumkumbatia mshambuliaji machachari wa Everton, Wayne Rooney. Hata hivyo kijana huyo aliachiwa muda mfupi baabaye baada ya Mwenyekiti wa Usalama wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuamuru kijana huyo kuachiwa baada ya jeshi la polisi kumshikilia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents