HabariMichezo

Mlipe pesa za Gadiel Michael – Zakazakazi amjibu Alikamwe

Baada ya Msemaji wa Yanga SC @alikamwe kumuandikia @zakazakazi ujumbe huu

“Wauza Ukwaju msijizime data. Majibu yetu ya Akaminko na Kipre vipi ?😄”

Naye Afisa Habari wa Azam FC @zakazakazi hakusita kumjibu Alikamwe

“Mdogo wangu @alikamwe, majibu mbona tulishatoa!!!!”

“Tulisema tuko tayari kukutana na nyinyi kulijadili hilo, lakini mnatakiwa kwanza mlipe pesa ya manunuzi ya Gadiel Michael mwaka 2017.”

“Hatuwezi kuongea biashara mpya leo wakati bado mna deni la zamani.”

“Lipeni kwanza lile deni, leteni hati ya benki kuthibitisha malipo, ndipo tuongee.”

Kumekuwa na vijembe vya hapa na pale kwenye kipindi hiki cha dirisha la Usajili la mwezi Januari likiwa linaelekea kufungwa.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents