Habari
Mnenguaji wa Twanga Pepeta Aisha Madinda afariki dunia
Mnenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Madinda amefariki dunia leo.
Taarifa kuhusu kifo chake kimedai kuwa mnenguaji huyo mahiri amefariki kwenye hospitali ya Mwananyamala. Zingine zinadai alifikishwa katika hospitali akiwa ameaga dunia tayari.
Bado haijafahamika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani. Taarifa zaidi zitakujia baadaye