Michezo

Mnyama ‘Simba’ auawa shamba la bibi: Nakuru,Gor Mahia zatinga nusu fainali ya SportPesa Super Cup

Klabu ya Simba SC Kutoka Tanzania imetolewa kwenye michuano ya kombe la Sportpesa Super Cup baada ya kugaragaza na Klabu ya Nakuru All Stars kutoka Kenya kwa magoli 5-4 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoshana nguvu dakika 90.

Kwa upande mwingine robo fainali ya mchezo wa kwanza wa leo uliochezwa kati ya Gor Mahia kutoka Kenya na Jang’ombe Boys kutoka Zanzibar,Gor Mahia imefuzu kutinga nusu fainali ya Sportpesa super Cup kwa kuichabanga Jang’ombe Boys goli 2-0.

Yanga yatinga nusu fainali ya SportPesa Super Cup Kibabe!!

Kwa matokeo hayo Klabu ya Nakuru All Stars itaungana na klabu ya Gor Mahia zote kutoka Kenya kucheza nusu fainali ya Kombe la Sportpesa Super Cup siku ya Alhamisi ya Tarehe 8-June wiki hii saa 10:00 jioni kunako dimba la uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Tiketi za michuano ya SportPesa Super Cup zaanza kuuzwa

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents