Siasa

MNYIKA: “Wabunge wa CHADEMA waliofutiwa uanachama walitoa maneno ya kashfa na kejeli” – Video

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetanganza kuwafukuza uanachama Mbunge wa Rombo Joseph Selasini na Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu kwa kuwa wamepoteza sifa ya kuwa wanachama wa chama hicho.

“Kamati Kuu CHADEMA imeazimia Wabunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wameendelea kutoka kauli za kejeli, kashfa na kukiuka maagizo ya Chama, hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama”

“Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama”

“Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, ilitakiwa awe mfano na kwakuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo”

“Kuhusu Wabunge wengine ambao wamekwena kinyume na maagizo ya Chama lakini hawajaonesha utovu wa nidhamu kwa kutoa kashfa kwa Chama, watatakiwa wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo” -John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents