Michezo

Mourinho: United lazima ishinde Europa League

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anahitaji klabu yake kuibuka mabingwa wa Europa League ili kumaliza mataji yote ya mchezo huo wa Mpira wa miguu. United imeshinda mataji yote kasoro taji moja pekee toka kuanzishwa kwa klabu hiyo Miaka Kenda iliyopita.

Taji pekee ambalo Mashetani hao wekundu hawajawahi kulitwaa ni taji hili la UEFA Cup ambapo bado inaonekana kuifanya klabu hiyo kuwa na doa pasipo kujua ni lini doa hilo litafutika. Kwa sasa United ipo nusu fainali ya kombe hilo ambalo wana njaa nalo kweli kweli huku mchezo wao wa nusu fainali ukitarajiwa kupigwa hii leo siku ya Alamisi dhidi ya Celta Vigo .

Katika Mkutano wake na waandishi wa habari, Mourinho alikuwa na hili la kuwaambia, “Huu ndio ubingwa pekee Manchester United haijawahi kuuchukua. Itakuwa vyema kama tutamaliza mashindano haya tukiwa tumefanikiwa kuuchukua katika Ulimwengu huu wa Soka,”.

“Kwa upande wetu, kama timu, tutakuwa tumepiga hatua nzuri pamoja na matatizo yote tuliyo kuwa nayo. Ushindi huo utatufanya kurudi tena katika mbio za kuwania Ubingwa Barani Ulaya Msimu ujao.

“Kwa sasa ni lazima tukubali tuna mitizamo tofauti kwa sababu Europa League ni jambo muhimu zaidi kwetu.
“Ligi ya Europa ina ushindani kwa muda mrefu. Klabu ambayo imefika hatua ya nusu fainali ni lazima ipite katika hatua ya makundi, Ambapo kuna timu hutoka na nyingine kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali na mnahitaji kufika fainali.”

“Celta imefika hapa wote tukiwa na lengo moja. Ni rahisi tu. Zilikuwepo timu nyingi na zenye ushindani mkubwa , timu zote zimetoka na zote zikiwa katika uwezo sawa.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents