Habari

Mwanamke ajitosa kinyang’anyiro cha rais Rwanda

Diane Rwigara, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya Urais nchini Rwanda katika uchaguzi utakaofanyika mwezi August.

                                              Diane Rwigara

Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda, Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita, na ana umri wa miaka 35.

Mgombea huyo wa kiti cha Urais amesema anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.

Akiongea na  waandishi wa habari, Bi. Diane Rwigara amesema lengo la mkutano huo ni kutangaza rasmi nia yake ya kugombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwezi wa 8 mwaka huu, huku akieleza sababu zinazomfanya kupigania kiti hicho.

”Kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuawa katika mazingira ya kutatanisha. Huwezi kusema kwamba uko katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi,” alisema.

Ameongezea kusema kwamba Rwanda hakuna uhuru wa watu kutoa maoni yao, na ni tatizo kubwa kwa wakosoaji wa serikali, masuala ambayo yeye anataka kubadilisha.

”Siasa isiyobagua kabila au tabaka fulani, ambayo inatoa fursa kwa kila Mnyarwanda na kumpa uhuru wa kutoa maoni yake. Nataka kuondoa dhana kwamba mtu akiwa na msimamo tofauti na serikali basi ataitwa adui wa taifa, hiyo nitaipiga vita katika uongozi wangu,” alisema Bi Rwigar

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents