Habari

Kalamu ya mwandishi itetee ukweli – Dkt Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe, amewataka waandishi wa habari nchini kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za uandishi katika kuandika habari zitakazoleta umoja huku wakisisitizwa kutumia kalamu ya uandishi vizuri.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe

Dkt. Mwakyemebe ametoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

“Uhuru wa habari una ukomo wake, hivyo ni muhimu kwa vyombo vya habari hapa nchini kuajiri watu wenye taaluma ili viheshimike kwa kutoa taarifa zenye kuzingatia maadili ya uandishi,” alisema Dkt. Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe alifafanua kuwa katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kalamu ya mwandishi wa habari itetee ukweli na si mambo ya haramu kwa sababu ya siasa au rushwa ambayo huwa kichocheo cha uvunjifu wa amani.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents