Habari

Mageuzi ya CCM ni dawa chungu – Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa (CCM), Humphrey Polepole ameyataja kuwa mageuzi yanayoendelea ndani ya chama hicho, kuwa ni dawa chungu kwa viongozi.

Kauli hiyo ilitolewa mjini Arusha jana na Polepole alipokuwa akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho kutoka wilaya ya Arusha.

Polepole alisema “Tunataka viongozi ambao hata asipokuwa na mshahara au umechelewa, fedha za chama ziendelee kuwa salama, tunataka viongozi wanaochukizwa na ubadhirifu wa mali za chama na Serikali.”

Aliongeza “Mageuzi ndani ya CCM ni dawa na kwa viongozi ni dawa chungu sana, lakini ni dawa. Kwa wanachama ni dawa tamu zaidi, kwa sababu wanaotuvuruga wakati mwingine ni viongozi hawa hawa,” alisema.

Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa CCM wilaya na Mkoa wa Arusha. Polepole alitumia fursa hiyo kuwaonya wanachama wenye mchezo wa kupanga safu za watu wanaotaka kugombea uongozi wakati wa uchaguzi kwa maslahi yao binafsi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents