Burudani

Mpoto awatembelea waliofukiwa ardhini kwa siku 41 Kahama

Mrisho Mpoto amewatembelea wachimbaji watano kati ya sita walionusurika kifo baada ya kufukiwa na kifusi kwa siku 41 katika mgodi huko wilayani Kahama walikolazwa.

11939499_921487764605111_371047303_n

Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM leo, Mpoto alisema ameguswa na suala hiyo la kustaajabisha.

“Nilikuwa Shinyanga sasa nikaona kwa sababu hapa Kahama ni karibu ngoja niwatembelee, ni kama sehemu ya ibada. Katika safari ya maisha kila kitu kinawezekana, usipokuwa waliongea sentensi moja kwamba ‘maiti za kwetu madini ya mwenye mgodi’, hiyo sentensi imenisikitisha sana,” alisema.

“Bado naendelea kuitafakari kwa sababu unavyosema maiti zenu madini ya kwetu maana yake naiona hii sauti ya nani? Ukiisikiliza sana hiyo sauti ni sauti ya mwenye mgodi, unaiona sauti ya mtu anayeumiliki mgodi. Ukiangalia huduma anazopata hata hawana insurance kabisa. Nafikiri serikali ya Magufuli inabidi iliangalie hili. Wakiwapa mikataba hawa watu watakuwa vizuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents