Habari

Mrisho Mpoto kuzindua studio yake ‘Waite’ Dec 29, itasaidia wasanii wachanga

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto December 29 mwaka huu anatarajia kuzindua studio yake mpya iliyopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam itayokuwa ikiwasaidia na kuwashauri wasanii wachanga

Mrisho-Mpoto2

Akizungumza na Bongo5 leo Mpoto, amesema pamoja na uzinduzi huo atazindua wimbo wake mpya ‘Waite’ ambao umetengenezwa katika studio hiyo na mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Kassim Majaliwa na wadau mbalimbali wa muziki nchini.

“Nimefungua studio kwa sasababu ya umri wangu umeenda sana,sasa kwenda kuweka foleni kwenye studio za watu inakuwa shida,pia nimefungua studio kawajili ya kuwasaidia wasanii wachanga. Kuna wasanii wengi wanataka kutoka ila hawana hela ya studio,kwahiyo sisi tutakuwa tunawashauri kimuziki nini wafanye. Nimemchukuwa AlLan Mapigo kwa muda wa miezi kadhaa kwAajili ya kusaidia ndoto za watu wengine,” Alisema Mpoto.

“Jina la Studio ‘Waite’ limekuja kutoka na wimbo wangu mpya ambao siku hiyo pia nitauzindua inaitwa ‘Waite’.Niliona ni wimbo wangu wa kwanza ambao umetengenezwa na studio hiyo nikaona bora hata jina la studio yangu niipe jina hilo hilo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents