Habari

Msaada Tutani: Mashabiki wengi wa Mr Nice wamshauri aachane na muziki, baada ya mambo kumuendea vibaya Kenya!

Lucas Mkenda a.k.a Mr Nice amekuwa katika midomo ya wapenda burudani Afrika Mashariki miezi kadhaa iliyopita baada ya kupata nafasi ya kufungua ukurasa mpya wa muziki wake nchini Kenya.

nice

Mr Nice mwezi July alifanikiwa kupata mkataba ‘mnono’ na label mpya nchini Kenya Candy n Candy ikiwa ni mwezi mmoja toka apoteze mkataba mwingine na label ya Grand Pa waliomchukua kwaajili ya kumrudisha kwenye ramani ya muziki baada ya kupotea kwa kipindi kirefu.

Sababu zilizotajwa na mmiliki wa Grand Pa za kusitisha mkataba wake na mwanzilishi wa style ya TAKEU, ni pamoja na uvivu, uzembe, ulevi pamoja na kukiuka masharti ya mkataba.

Hata hivyo siku chache zilizopita mkurugenzi wa Kampuni ya Candy & Candy Records, Joe Kariuki aliiambia MWANANCHI kuwa kampuni yake imetofautiana na Nice kutokana na mwanamuziki huyo kushindwa kufuata muongozo wa kampuni, kitu ambacho kingepelekea kampuni kuingia hasara.

Kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Radio jana walikaribisha mashabiki wa Mr Nice kumsaidia kwa ushauri na maoni katika kipindi hiki ambacho mambo yanamuendea vibaya.

“Mr.Nice ni mmoja kati ya wasanii ambao walishawahi kufanya vizuri na kupotea, leo Kameta producer ambaye alimtoa amesema jamaa anahitaji msaada wa kisaikolojia kutokana na hali aliyokuwa nayo sasa hivi. Je, unapenda kumshauri nini Mr. Nice?”

Haya ni baadhi ya maoni na ushauri wa mashabiki kwa Mr Nice:

Leonard Mbuya Aache gambe na apige kazi mchaga gani ww unapenda starehe ivyo arawaaa? Leonard Mbuya nipo ubungo.

William Chingafirst yaani ukichezea nafasi huwezipata tena, asahau kuwa kama awali, tayari akina platnum wameziba, jamaa alikuwa mbali lakini kachezea bahati

Hosea John ARUDI KWA KAMETA ILI AMUWEKE SAWA TENA MAANA MR NICE ALIJAWA UJINGA BAADA YA KUTOKA..

Emmanuel Mwakyusa SI MR NICE ni wasanii wengi tuu na watanzania wa maisha ya CHINI wako kwenye hali ngumu

Mhagama Edwin Kufulia kubaya, inabid atembeze bakuli wadau tumchangie hahaha kwa MTONYO gan

Awadh Z Chemen Kma kna klev ana2mia ajarb kuacha na kuwafarj wazaz wke

Suleyman Sexbody Tatizo nyimbo zawatoto zimekwisha,

Rick Johnson Afungue duka lolote akae auze mwenyewe,mziki ushakuwa ugonjwa kwake utamliza kila siku

Shaffi Khanain Sijapenda ushauri wenu marafiki kama una ushauri nyamaza 2 yeye nibinadam nasio malaika kakosea mwanzo kwasasa nikumuombea mungu arudishe afya yake nakufanya kazi 2

Henry Alex Lwinga duuh!!watanzania hawana la maana lolote tumeambiwa tumsaidie kisaikolojia but i thnk was uneducated pple ambao wanatoa coment za kizush eti ajiunge na freemason kama watoto wa la pili vle just thnk twice n toa coment xo kulopoka tu ili ujulikane

Razz Remedy kipindi cha kuimba nyimbo za watoto kimeisha,sio kwamba hawez kuimba ila ameshindwa kuenda na soko,pombe mbona wengi wanatumia

Artist Ackshuba kampan yake ya zaman ndio inayomtesa nice, yaan kama watu wake aliyekuwa anatumia nayo hela zake wakimrudia, ninaiman #nice atakaa na akashaurika ila bila hawo, kiukweli hawez tulia kiakili

Denis Joseph Ijumba Dah ! Inauma but ndo ishatokea akae chin ajipange maisha safara ukianguka unacmama unajifuta unaanza kukimbia mbio kali kwa mikakati sahihi ili ucje ukajikwaa tena, think twce ma broo u still kijanaaa

Artist Ackshuba mr nice anachohitaj ni msaada mkubwa wa mawazo wala sio hela, maana hela alizowah kuzishika afu zikapotea, hilo ndilo tatizo kubwa

Chad Sanga Ande kwa diamond platnum rais wawasafi akapige magoti ashauriwr mziki unaendaje bongo ili ajipange au kamavp akajiunge na waliogulia wenzie kina dullysykes Tid mr.blue qchila wadiskas watoke vp labda watanzania watawaelewa aise koz huyo jamaa kachezea sana mtama LMAO

Tawfiq Red Arxy Siwa Aache mashauzi kwani kakutanishwa na watu then anaanza nyodo ilikuwa kunaulazima gani wakumjibu nyodo yule mc kule kenya?

Ariana Traves Kaka anaweza la msing abadilishe muondoko.

Emanuel Adebaryor Minde Harudi Kwenye Muziki Kama Zamani Na Atatoka Tu, Mwambie Apoteze Maneno Ta Watu Wasemayo, Afuatilie Ya Kwake Na Atatoka, Asikate Tamaa Kila Jambo Linawezekana, Kuto Dsm Emmanuel Minde

Emma De Andrew mbona mi nilisikia kuwa yuko kenya ana amechukua mkataba na maplodwiza wa huko mambo yake safi leo tena kafulia

Katuga Ally ni moja ya kichwa hatari sana tz naukubali sana angekuwepo kwenye game hadi now diamond akasome……wamsaidie panapo itajika msaada…

Raphael Sama KWA WASANII WETU WA BONGO UKIWAAMBIA UKWELI UANONEKANA UNATAKA UMAARUFU. NI KWELI WENGI WANAUMWA KISAIKOLOJIA ILA NDO HAWANA UTAYARI KUPOKEA USHAURI. Hongera Kameta

Mohamed Mlunga wabongo mnapenda kumona mtu anapata tabu,,,na kukaa na kuaza kumcma vbya,,,,,ibu ona mnafurahi kuona mwenzenu anatecka,,,,,toa mchango wako wa mawazo na kejeli,,,,

Peter Jully Mdee atulie ajipange kama ni hela haznaga ndugu hasa pale unapotaka kwenda kasi nazo mwishoe znakuumbua..jipange na mishe nyingne kuhusu mziki sikushaur mana game ni ngumu c kama kipndi kile.

Claud Magesa Ajipange upya tena. achane na disi za washikaji mungu atamusaidiya

Habibu M Faraji Kwasasa wasanii wanaimba nyimbo za kikubwa, na kwakuwa wewe nyimbo ni kama ukuti ukuti ukuti wa mnazi zote umemaliza sasa ktk game ngumu hii utaimba nini tena?

Papy Benshi MR NICE nimsani mzuli hatawatu wanadai kama amepotea naamini uwezo anao namaanishi wakimziki pia anamashabikiwake kinachotakiwa aweze kujituma kamazamani

Mhandeni Sonyo Huyu ni jembe. Anopange upya
Mungu atamsaidia si unajua mchaga mzaramo hashindwi atulize bongo na tamaa hasa ya madenti. Hawaishi kIla sikuwznaziwa design mpya

Joyce Mrina Alianguka ameinuka ajipanguse mavumbi na aendelee na safari….. Akumbuke asili yake, asaidie wazazi wake na kujiweka karibu zaid na familia….. Jiulize wewe unaemshaur afanye ujinga ingekuwa ww ndo unaambiwa hvyo au kukashifiwa ingekuwaje? Kilichomtokea Mr Nice chaweza kumtokea yeyoteyule hivyo tujichunguze kbla ya kuropoka hovyo… Domo liliponza kichwa jamani…. Big up mr nice bado unaweza…..

Mudy Gumbo Daa inabidi asubili sana maana fungu lake lilisha pita na akalichezea kwahiyo awe mpole asubiri mzunguko mwingine kama kapangiwa kutoka tena atatoka2 lkn kama ndio majanga basi majangatu

Iddi Mbilu starehe zakuwafurahisha watu siku zote nishimo laumasikini”sasa shimo alichimbamwenyewe nakaingia mwenyewe iweje tena atake msaaada?

Diberatus Rujangi Ashakula dawa zake na hayo ndo matokeo yake,nafikiri kuwe na semina elekezi kwa wasnii maana hawatuwakilishi ilivyo

Diberatus Rujangi Ashakula dawa zake na hayo ndo matokeo yake,nafikiri kuwe na semina elekezi kwa wasnii maana hawatuwakilishi ilivyo

Mawazo Sharifu Aisee Huyu Jamaa Kiukweli Ni Mlevi Sana.Hata Mm Mara Ya Mwisho Nilikutana Nae Mombasa Yupo Chakali.Kwan Wakati Ana Hela Alishawahi Kuja Studio Kuomba Ushauri Jins Gan Atumie Pesa Zake?Awatafute Wachaga Wenzake Awapige Kopo?Tutasaidia Wasojiweza Lakn Sio Mlevi

Elias Martin Me namshauri aache music ili afanye mishe zngine coz kila kitu na time yake.

Hamza Ngualo Kameta ndiye hasa anamjua Mr. Nice it’s better akamrudisha afanye nae kazi like Man Walter na 20 Percent.

Costantine Ndagala Hakuna snitch kama pesa,ukizipata fanya vya maana/Maana zikisepa utazitafuta usiku na mchana.

Mússä Kägäwä Ajigundue kwanza yeye n nani alfu ajijue anafanya nini alfu ajipange ktoka upya akifanya hvyo m nadhan atafanikiwa coz jamaa anaweza m namkubali kiupande wang

Hassain Kigumi mr nice tatizo lake anaimba nyimbo za watt ambazo azina soko kama kashindwa mziki aludi kijiji akalime,nauri 2takuchangia kiroo safi.

Imanuel Kasumbi Mr. Nice tulia kuishiwa sio kufa, ebu tuliza kichwa fanya mambo mengine kwanza mziki uache kidogo ujipange njua utafanya vizuri hata badae ila tafuta maisha mengine kwanza usiogope watu kusema iyo kawaida!…….hata mpanda ngazi hushuka na kuanza moja rudi nyuma kwanza ujipange.

Nindey Balcazar Chicharito afanye issue nyingine kwenye maisha! mziki umebadilika sana kwa sasa hauwezi.,kila kitu kina wakati wake

Nimrod Roosebert arudi tz make naskia yuko kenya afu atulie asiwe na dharau kwasababu wasanii wengi wa kibongo wakipata kidogo matako yanalia mbwata

umanne Dinongo STAREHE INATAKIWA KWA MPANGILIO,ukipewa wewe basi ujue kuna mtu kanyimwa,

Danstarn Chacha Mallegs Namwambia asikate tamaa abadilishe staili ya mzki anaoufanya hiv sasa! Maana tme hii ni digital! I m danstarn2 chacha from Kenya

Stanley Kilawe ni kweli pole sana kaka but hata sijapendezewa na ww hapa bongo una mashaiki alafu unaenda kenya ina maana ss umetuzarau au?

Mawazo Sharifu Hakujipanga Kipindi Ana Hela,sasa Kafulia Ndo Anaanza Kusumbua Watu.Kaenda Kenya Lakin Full Kuvuruga,sasa Huyu Ni Mtu Asiejifunza Pale Alipojikwaa?Kweli Stress Can Be Created By Person.Alijitakia Mwenyewe Na Hii Iwe Mafundsho Kwa Wasanii Wanang’ara Hiv Sasa

Mawazo Sharifu Alikuwa Akiwaimbia Watoto Kipndi Kile Lakni Sasa Wameishakua Watu Wazma.Asubiri Wazaliwe Watoto Wengne.Matoto Yenyewe Ya Digital Atayaweza?Sasa Yanapga Kwaito

Eng Hongera Na hawa watoto wanaokurupukia muziki sasa hivi na kukimbia shule hii ndio mifano halisi wanayotakiwa kujifunzia,wakati waliowatangulia kwenye game wanarudi shule,yeye form one anakimbia shule,hujui kuna muda game itakugomea na kama huna kitu kingine cha kufanya ndio unaishia kuvuta unga.Nadhani haya ameyazungumza vizuri kabisa “NIKKI MBISHI” kwenye track yake ya “NYAKATI ZA MASHAKA”…,

Elia Baraka Boma TOKA MVUMI MAKULU DODOMA.POLE SANA MR.NICE KWA YALIYO KUKUTA NA JIPANGE KWA MAISHA MAPYA HUKU MTAAN.NAJUA HUPENDA YATOKEE YALIYO KUKUTA ILA KWA HALI ULONAYO HIVI SASA NI YA KUJIFUNZA KUWA MAISHA NI KUWEKEZA……

Imanuel Kasumbi Mr. Nice tulia kuishiwa sio kufa, ebu tuliza kichwa fanya mambo mengine kwanza mziki uache kidogo ujipange njua utafanya vizuri hata badae ila tafuta maisha mengine kwanza usiogope watu kusema iyo kawaida!…….hata mpanda ngazi hushuka na kuanza moja rudi nyuma kwanza ujipange.

Je wewe na wewe unaushauri gani wa kujenga kwa Nice?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents