Habari

Msechu azawadiwa Bima ya Afya

Msechu azawadiwa Bima ya Afya

Kampuni ya bima ya Resolution Health Afrika imemzawadia mshiriki wa Tusker Project Fame 4, Peter Msechu zawadi ya bima ya afya kiwango cha Premier Plan kutokana na mafanikio yake katika mchezo alioshiriki mwishoni mwa mwaka jana.

Msechu azawadiwa Bima ya Afya

Meneja Mkuu wa Resolution Health Afrika Mashariki, Oscar Osir, alimkabidhi Msechu zawadi hiyo katika hafla iliyofanyika ndani ya ofisi kuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Peter Msechu aliipongeza kampuni ya bima ya afya Resolution Health, kutokana na zawadi aliyopokea toka kampuni hiyo ya Bima ya Afya ambayo itadumu mwaka mzima wa 2011.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents