Promotion

Mshindi wa milioni 1/- kupitia promosheni ya JayMillions akabidhiwa kitita chake

Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeledeshwa na Vodacom Tanzania amemkabidhi kitita cha shilingi Milioni 1/- mshindi wa promosheni hiyo Claudia Mapunda ambae ni mkazi wa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alikabidhiwa fedha zake katika hafla fupi iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

001
Balozi wa promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ‘Zembwela’na Claudia Mapunda(kulia)ambaye aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi milioni 1/-kupitia promosheni hiyo wakihesabu fesha hizo kabla ya Balozi huyo kumkabidhi rasmi kitita chake katika hafla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Katika hafla hiyo Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud”‘Mr.Jay’ ambaye alimkabidhi mshindi fedha hizo alikuwa kivutio kwa watu wengi ambao walisimama kwa muda kufanya shughuli zao kwa ajili ya kumsikiliza ambapo aliwataka wachangamkie fursa ya kujishindia mamilioni ya fedha kwa njia rahisi ya kutuma neno JAY kwenda namba 15544 kucheki kama wameshinda.

Promosheni ya Jaymillions inayoendelea ikiwa katika wiki ya sita na ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha.

004
Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 1/= kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Claudia Mapunda(kulia) akifurahia kwa kuonesha kitita chake cha fedha alizoshinda baada ya kukabidhiwa na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud ‘Zembwela’(kusho) anaeshuhudia katikati ni mpambe wa Balozi huyo Maria John.Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Hadi kufikia leo ni Sh. 134m/- pekee zilizokwisha kuchukuliwa na Uwezo Madengenya na washindi wengine wawili – Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa na James Mangu (Mwanza) – wa Sh. 10m/- na milioni 11m/- zimekwenda kwa – Chiliphod Wanjala (Mwanza), Janeth Nganyange (Njombe), Evarista A (Mwanza), Stanley Bagashe (Shinyanga), Ramadhani H. Maulid (Dodoma) na Lucas Masegese (Shinyanga),Ayubu Makonde(Mbeya), Hyasinti Mlowe(Njombe), Florian Gwayu(Arusha), Modesta Milanzi(Ruvuma), Nobert Minungu(Dodoma), Busolo Swaleh(Arusha), Claudia Simon Makunda(Dar es Salaam) na Gerald Shao(Kilimanjaro)– wa Sh. 1m

Akizungumza wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa Shilingi Milioni 1 wa Promosheni hiyo, Claudia Mapunda, amewaomba Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Kampuni ya Vodacom nchini katika kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania.

“Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha,” alisema Claudia.

Claudia ambaye ni mwajiriwa akiwa kama karani katika kampuni anayofanyia kazi amesema fedha hizo zitamuwezesha kuanziasha mradi wa ufugaji wa kuku ambao amekuwa akiwaza kuuanzisha kwa muda mrefu “ fedha nilizopata nitafungua mradi wa ufugaji pia zitanisaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili familia yangu.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akiongea katika hafla hiyo alimpongeza mshindi huyo na kusema kwamba fedha hizo zimeenda kwa mshindi sahihi kwani mshindi huyo ana malengo mazuri ya matumizi ya fedha zake kwa kuanzisha mradi wa ufugaji kwa ajili ya kuinua kipato cha familia yake.

Pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents