Habari

Mtoto wa Lowassa amcharua Waziri Kigwangalla ajibu ‘tusubiri muda ufike’

Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe Edward Lowassa, Fredrick Lowassa amemuashia moto  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Hamisi Kigwangalla kwa kumwambia kuwa matamko yake mengi anakurupuka.

Fredrick Lowassa na Waziri Kigwangalla

Fredrick Lowassa ametoa kauli hiyo baada ya tamko la Waziri Kigwangalla kutaka ploti namba 4091 iliyopo Njiro jijini Arusha kuchunguzwa kwani eneo hilo la ardhi ni mali ya Serikali na nusu ya eneo hilo tayari limevamiwa kinyemela na watu binafsi na kuagiza kamishna wa ardhi kufanya uchunguzi juu ya umiliki wa watu hao.

Nimesikia taarifa za Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha. Nimesikitishwa sana na matamshi hayo kutoka kwa waziri ambaye kwa mtu mwenye wadhifa wake kutoa kauli zisizo na msingi wowote na kulaghai Umma,“amesema Fredrick Lowassa kwenye taarifa yake aliyotoa kwenye vyombo vya habari na kumuelezea Waziri Kigwangalla.

Nimemfahamu Mhe Kigwangalla kwa miaka mingi, tangu wakati anavurugana na mbunge mwenzake wa Nzega na rafiki yangu Mhe Hussein Bashe kule Nzega,  Kwa maoni na mawazo yangu nimekuwa nikiamini kwamba Kigwangalla atakuwa mtu aliyebadilika na kujifunza kutoka na makosa yake ya nyuma. Kauli yake ya leo ni ushahidi kwamba bado ana matatizo yale yale ya kukurupuka. Ni wazi hata baada ya mambo mengi kubadilika na pengine nyakati za kuchafua watu kukoma, ndugu huyu bado anaishi nyakati zile zile. Ni wazi Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais Magufuli , kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina Wataalamu na uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote, Nikiwa kama Msemaji wa Familia ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa,“amemaliza Fredrick Lowassa.

Hata hivyo Waziri Kigwangalla amemjibu mtoto wa Lowassa kuwa yeye kwenye taarifa yake hakumtaja Lowassa wala Fredrick Sumaye bali alitaja eneo hilo la Njiro kuchunguzwa umiliki wake.

Mhe. Kigwangalla amesema huu ni muda wa kukaa kimya na kusubiri tamko rasmi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Lukuvi juu ya uhalali wa umiliki wa eneo hilo.

Tumetoa agizo ambalo litataka Kamishna wa ardhi atupe ufafanuzi kuhusu uhalali wa umiliki wa eneo lile kwa hiyo tunasubiria, lakini nilichokisema leo ambacho kimenishangaza kidogo kuona kwamba kama vile nimetafsiriwa nimetaja majina ya watu wanaomiliki pale akiwemo Mzee Lowassa nimeona mwanaye ndugu Fredrick Lowassa ametoa tamko. Mimi sikutaja mtu yeyote juu ya umilikia wa lile eneo,“amesema Waziri Kigwangalla na kusisitiza.

Nimeamua kutoa maelezo haya ili ndugu yangu Fredrick Lowassa asitokwe povu sana tusubiri muda ufike“.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents