Habari

Muhimbili yapokea msaada wa taulo za watoto zenye thamani ya Milioni 35 kutoka DOWEICARE

Muhimbili yapokea msaada wa taulo za watoto zenye thamani ya Milioni 35 kutoka DOWEICARE

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imekabidhiwa msaada wa taulo za watoto wachanga aina ya Softcare zenye thamani ya TZS. 35Mil kutoka kampuni ya DOWEICARE ili kusaidia watoto waliozaliwa na watakaozaliwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia sasa.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza DOWEICARE kwa mchango huo ambao utasaidia kina mama na watoto wao hasa wasio na uwezo wa kumudu kununua taulo hizo mara tu wanapojariwa kupata baraka za watoto.

“DOWEICARE mmeonesha kujali kwani taulo hizi zitasaidia katika kutunza na kuandaa afya ya mtoto ambaye siku za usoni atakuwa kiongozi mwenye mawazo chanya na akili njema itakayotumika katika kuliongoza taifa letu kwani mara nyingi tumekuwa tukitoa msaada kwa watu wazima na kusahau kuwa watoto ni watu muhimu katika jamii hasa katika kuandaa taifa imara na bora lenye maendeleo makubwa,” amesema Mh. Chalamila.

Akipokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi ameishukuru kampuni hiyo na kuwaomba kuendelea kuunga mkono hospitali kutokana na kuhudumia wagonjwa wengi na wenye vipato tofauti.

“Tunajua nyie niwatengenezaji wa bidhaa muhimu ambazo tunahitaji zaidi katika kuwahudumia watoto hivyo ombi letu kwenu ni kuwa tunaomba hapo baadaye mtuuzie bidhaa hizi kwa bei ya punguzo kwani kufanya hivyo mtakuwa mmewasaidia watoto wachanga wanaozaliwa na kuhudumiwa hospitalini hapa,” amesema Prof. Mohamed.

Aidha Profesa Janabi amesema kwa siku katika hospitali hiyo wanapokea watoto 100 kwa wiki 379 na kwa mwezi 1500.

“Tunapokea watoto hadi wenye gramu 800 lazima kuwepo na uwekezaji mkubwa tunafanya huduma kwa wagonjwa wa ndani na wan je wapo madaktari bingwa wa watoto wa saratani, kisukari, tumbo na kupungukiwa damu, jengo hili la watoto linafaa kuwa hospitali kamili ya watoto kwa sababu lina vigezo vyote wakiwemo madaktari bingwa”

Naye Balozi wa Softcare brand, Zarina Hassan maarufu “Zari the Boss Lady” ameitaka jamii kutambua umuhimu kwa kuitunza afya ya mtoto kwa kutumia bidhaa zenye ubora na kusema kuwa taulo za Softcare zina ubora wa hali ya juu na salama kwa watoto wachanga.

Aidha amesema yeye kama mzazi anatambua changamoto ambazo wamama wengi wanazipitia wakati wa kujifungua na malezi, hivyo taulo hizo zitakwenda kuwasaidia watoto waliopo katika hospitali hiyo.

bKwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Doweicare, Victor Zhang, amesema kampuni yao imeamua kuwa mshirika wa serikali katika jitihada za kuwezesha familia za kitanzania kuwa na afya bora.

“Tunaamini kupitia jitihada hizi tutakuwa tumeunga mkono maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuona watoto ambao ni taifa la kesho wanapata huduma bora za kiafya,”alisema Zhang na kuongeza kuwa:

Amesema wamechagua hospitali ya Muhimbili kwa kuwa ni kituo kikubwa cha matibabu nchini na wanaamini msaada huo ni mwanzo mzuri wa ushirikiano katika sekta hiyo muhimu.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents