Habari

Muswada wa Habari hautomfukuzisha mwandishi asiye na shahada – Habari Maelezo

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Hassan Abbas amesema kuwa waandishi wa habari hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu muswada wa huduma za habari kwakuwa hakuna atakayefukuzwa wala kuachishwa kazi kwa kigezo cha kutokuwa na elimu ya shahada ya kwanza.

oth_7838

Abbas ameyasema hayo Jumanne hii katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV. Amesema waandishi hawana haja ya kuuogopa muswada huo, badala yake wausome na kuuelewa.

“Sheria itatoa kipindi cha miaka 5 ili watu wajiendeleze katika taaluma hii ya habari. Hivyo hakuna mwandishi wa habari atakayefukuzwa wala kuachishwa kazi kwasababu ya huu muswada kwa vile lengo ni kuwaandaa waandishi ili waweze kufanya kazi vizuri kwa kuzingatia taaluma,” alisema.

Aidha Abbas aliongeza kuwa kigezo cha taaluma kwa waandishi wa habari hakitaainishwa katika sheria bali katika kanuni.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents