Burudani

Muziki wamfanya Stamina ashindwe kumaliza chuo

Msanii wa muziki wa Hip Hip kutoka Morogoro, Stamina amedai ameshindwa kumaliza chuo kwa wakati kutokana na kubanwa na shughuli za muziki.

Rapa huyo ambaye alikuwa akisomea Bachelor Degree in Industrial Relations, katika chuo cha ustawi Posta, ameiambia Bongo5 kuwa, kwa sasa anaendelea na degree yake mkoani Morogoro.

“Bado nasoma namalizia Degree yangu Morogoro, hapa Ustawi sikumaliza,” alisema Stamina. “Sisi wasanii tunakuwa busy sana na masuala ya muziki na kusoma kunahitaji muda wa zaida. Lakini ninashukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri hata hivi karibuni nilikuwa kwenye mitihani,”

Rapa huyo amedai ameamua kusoma ili awe na plan B nje ya muziki wake.

“Unajua kuna wakati unafika unatakiwa ufanye kitu zaidi ya kimoja, muziki ni sehemu ya maisha yangu lakini lazima niwe na kitu ambacho naweza kufanya nje ya muziki,” alisema Stamina.

Katika hatua nyingine rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa albamu yake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents