Uncategorized

Swahiba wa ‘El Chapo’ atiwa nguvuni nchini Mexico

Swahiba wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya duniani na Kiongozi wa kundi la Sinaloa Cartel, Joaquin Guzman maarufu kwa jina la ‘El Chapo’ amekamatwa jana nchini Mexico.

Image result for damaso lopez
Damaso Lopez katikati akiwa chini ya uangalizi mzito mapema baada ya kukamatwa na Polisi nchini Mexico.

Mamlaka nchini Mexico zimesema kuwa Damaso Lopez rafiki yake na ‘El Chapo’ alikamatwa katika mji wa Mexico City kwa tuhuma za kusafirisha tani za Madawa ya kulevya kwenda nchini Marekani.

Tangia kukamatwa kwa aliyekuwa kiongozi kundi hilo Joaquin Guzman ‘El Chapo’, viongozi wa juu wa kundi maarufu linalojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya la Sinaloa Cartel, limekuwa likisambaratika kila kukicha kwa kung’ang’ania madaraka hali iliyopelekea kuibuka kwa uhalifu katika maeneo ya Sinaloa,nchini Mexico.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents