Habari

Mvua kubwa kupiga Dar kuanzia kesho, TMA yatoa tahadhari 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetangaza kuwepo kwa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika ukanda wa Pwani kuanzia tarehe 3 Disemba 2021 hadi 5 mwezi huu.


Taarifa ya TMA iliyotolewa mkoani Dar es Salaam imeeleza kuwa licha ya mvua hizo kubwa kumalizika tarehe 5 Disemba 2021, mvua za kawaida zitaendelea hadi mwezi Aprili mwaka 2022.

Kufuatia uwepo wa mvua hizo, TMA imewataka Watanzania wote kuchukua tahadhari hasa kwa mvua zinazoambatana na radi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents