Habari

Mwaka 2023 utakuwa mgumu zaidi kiuchumi kuliko 2022- IMF

Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF limesema kuwa uchumi wa dunia utakabiliwa na wakati mgumu zaidi mnamo mwaka huu wa 2023, wakati ambapo mataifa makubwa yakishuhudia shughuli zao zikidhohofika.
Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva alipokuwa akihojiwa jana na kituo cha habari cha CBS, alisema mwaka huu wa 2023 utakuwa mgumu kuliko mwaka uliyopita kwa sababu mihimili ya uchumi wa kimataifa ambayo ni Marekani, Umoja wa Ulaya na China, zinashuhudia kwa wakati mmoja kusuasua kwa shughuli zao.

Mwezi Oktoba, IMF ilipunguza matarajio yake kwa ukuaji wa uchumi wa kimataifa kwa mwaka 2023, kutokana na kuendelea kwa vita nchini Ukraine pamoja na shinikizo la mfumuko wa bei na viwango vikubwa vya riba vilivyobuniwa na Benki Kuu ya Marekani kwa lengo la kupunguza makali ya mfumuko wa bei.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents