Habari

Mwanafunzi wa darasa la 6 akutwa amefungiwa ndani na mwanaume akimlazimisha kumuoa, Mwanafunzi huyo asimulia ilivyokuwa – Video

Mwanafunzi wa darasa la 6 akutwa amefungiwa ndani na mwanaume akimlazimisha kumuoa, Mwanafunzi huyo asimulia ilivyokuwa - Video

Uongozi wa mtaa Geita mjini kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hilo  wamemkamata  mwanaume aliyekuwa anaishi na mwanafunzi wa darasa la sita kwa kumlazimisha kumuoa.

Akizungumza jinsi tukio hilo lilivyotokea wifi wa mwanafunzi huyo,  Bi Magret sabuholo  amesema kuwa yeye alimuacha nyumbani nakuelekea sokoni mida ya asubuhi lakini baada ya kurudi akitoka sokoni hakumkuta na alimuulizia hadi ilipofika usiku hakuonekana ndipo  hofu Ilitawala  hali iliyowapelekea kutoa taarifa kwa uongozi wa mtaa huo .

Kwa upande wa kaka wa mwanafunzi  huyo Bw Siajari Samsoni amesema kuwa mdogo wake alikuja kwa lengo la kumsalimia kutoka katika kjijij  cha Samva kata ya Nyakabango wilaya ya Mleba  mkoani Kagera kwani  alikuwa  amefunga shule.lakini amesikitishwa sana na tukio hilo ambalo limetokea katika familia yake.

Mbali na hilo Mwenyekiti wa mtaa Geita mjini Bw  salvatory Danielly amesema kuwa mara baada ya kupokea taarifa hizo alichukua jukumu la kuandika barua ili kuelekekea katika kituo cha polisi kwa ajili ya kupata msaada wa kwenda kuwakamata.

Bongo5 ilipata nafasi ya kuzungumza na binti  huyo  mara baada ya kutoka hospitalini ambapo ameeleza kuwa mwanaume huyo alimshawishi kuwa atamuoa endapo atamkubalia.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents