Habari

Mwanaharakati atinga Mahakamani na hoja nzito, Ataka ukomo wa Rais kuongoza nchi kwa mihula miwili ufutwe

Mtanzania Patrick Dezydelius Mgoya, mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam amefungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania akihoji uhalali wa kifungu cha 40(2) cha katiba ya nchi, ambacho kinachotoa ukomo wa kipindi cha Urais.

Katika kesi hiyo, Mgoya ameiomba mahakama kutoa ufafanuzi wa kina na athari za kifungu hicho cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mgoya ameiomba mahakamani kutoa ufafanuzi sahihi wa kisheria na wa kina kwa kifungu cha 42(2) cha katiba, na namna kinavyohusiana na vifungu namba 13, 21 na 22.

Kifungu namba 13 kinazungumzia usawa mbele ya sheria, Namba 21 kinaelezea uhuru wa kushiriki shughuli za umma huku namba 22 kikielezea haki ya kufanya kazi.

Mgoya ameiomba mahakama kutoa ufafanuzi wa kifungu namba 40(2) kwa pamoja na kifungu namba 39 ambacho kinaelezea sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais.

Katika hoja zake, Mgoya amesema kuwa kwa kuweka ukomo wa kipindi cha Urais, kifungu 40(20) kinakiuka vipengele vingine vya katiba ambavyo vinatoa uhuru kwa wananchi kushiriki katika shunguli za umma.

Kesi ya hiyo ya Mgoya imekuja katika kipindi ambacho Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza kuwa hana lengo la kubadilisha katiba ili aendelee kuwepo madarakani, na kwamba muda wake utakapomalizika, hatoongeza hata dakika tano kwani anaheshimu katiba ya nchi na chama cha CCM.

Chanzo:https://swahilitimes.com/2019/09/02/patrick-mgoya-afungua-kesi-mahakama-kuu-kupinga-ukomo-wa-urais/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents