Burudani

Mwanamitindo anayetakiwa kulipwa dola milioni 100 za talaka apata kikwazo hiki!

Mwanamitindo wa zamani, Christina Estrada, aliyeshinda kesi ya kulipwa dola milioni 100 za talaka na bilionea wa Saudi Arabia, Walid Juffali, atalazimika kusubiri kabla ya kupewa mtonyo wake.

christina-estrada

Mahakama ya jijini London iliagiza fedha hizo ziwe zimelipwa hadi Ijumaa hii, July 29, lakini Juffali alifariki kwa saratani baada ya maamuzi hayo. Malipo hayo yatachelewa wakati mambo yanawekwa sawa.

Estrada ambaye ni mzaliwa wa Marekani alihitaji kulipwa kiasi hicho kikubwa cha fedha ili kumwezesha kuishi maisha yake ya kifahari ikiwemo mijengo anayoishi Saudi Arabia, Beverly Hills, Venice na Switzerland. Gharama zingine ni $140,000 za nguo za kushona, $27,000 za viatu na $50,000 za makoti ya manyoya.

Aliambia mahakama kuwa huwa anaalikwa mara nyingi kwenye sherehe za kifalme Ulaya. Juffali alimpa talaka Estrada mwaka 2014 bila kumpa taarifa inayoruhusiwa na sheria za Kiislamu. Baadaye alipewa ruhusa ya kumshtaki mumewe nchini Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents