Michezo

Kombe la FA la Uingereza kuanza kuitumia sheria ya wachezaji wanne wa akiba

Shirikisho la soka Uingereza (FA) limepanga kuziruhusu timu za nchi hiyo kuanza kuwatumia wachezaji wanne wakati wa dakika 30 za nyongeza kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la FA msimu ujao.

_90529828_gettyimages-465709268

Michuano hiyo ya kombe la FA inatarajiwa kuanza Agosti 5 mwaka huu ikizishirikisha timu za ligi kuu ya Uingereza na zile zilizopo daraja la kwanza.

Sheria hiyo ya kuwabadilisha wachezaji wanne kwa mara ya kwanza iliweza kujaribiwa kwenye mashindano ya Copa America yaliyomalizika mwezi Juni mwaka huu.

Aidha sheria hiyo inatarajiwa kupitishwa na chombo chenye mamlaka ya kubadili Sheria za Soka (IFAB-International Football Association) ili sheria hiyo iweze kutumika pia mpaka kwenye michuano yote iliyokuwa chini ya Fifa ikiwemo kombe la dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents