Michezo

Mwanamke aliyeshinda dola milioni 26, aifua tiketi ya kupokea fedha bila kujua

Mwanamke mmoja anayedai kununua tikiti ya ushindi kwa droo ya Bahati Nasibu ya $ 26m (£ 18.5m) sawa na Tsh bilioni 60,276,164,000ya California anasema aliiacha kwenye mfuko wa suruali na kuiharibu wakati akiifua suruali hiyo, vyombo vya habari Marekani vimeripoti.

Tiketi ya ushindi ya SuperLotto Plus iliuzwa katika duka moja katika kitongoji cha Los Angeles huko Norwalk mwezi Novemba.

Mwanamke huyo, ambaye hajatajwa jina, aliripotiwa kunaswa na CCTV akinunua tiketi dukani wakati huo.

Lakini tarehe ya mwisho ya kupokea zawadi kubwa ilipita siku ya Alhamisi.

Waandaaji wa bahati nasibu wanasema mshindi lazima apatikane ndani ya siku 180 za droo, ambayo ilifanyika tarehe 14 Novemba

Mfanyakazi katika duka huko Norwalk, Esperanza Hernandez, aliliambia gazeti la Whittier Daily la California kwamba mwanamke huyo alikuwa amemtembelea Jumatano akidai kwamba ndiye mshindi wa tiketi, lakini kwamba alikuwa amepoteza tiketi na kwamba kwa bahati mbaya aliifua pamoja na nguo

Msemaji wa Bahati Nasibu ya California, Cathy Johnston, aliliambia gazeti kwamba picha za CCTV za duka hazitatosha kuthibitisha madai ya mwanamke huyo, na kwamba “uthibitisho muhimu wa tiketi hiyo ulikuwa unahitajika

Hatahivyo, nakala ya video hiyo imepelekwa kwa waandaaji wa bahati nasibu na dai hilo linachunguzwa zaidi, Bi Johnston alithibitisha.

Ikiwa hakutakuwa na mshindi kiasi hicho cha fedha kitagawiwa kwa shule za Umma za jimbo la California, waandaaji wameeleza kwenye taarifa yao. Muuzaji aliyeuza tiketi ya ushindi amepokea $ 130,000 kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa bahati nasibu, iliongeza taarifa hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents