Habari

Wadukuzi Marekani wanalipwa na Serikali kudukua, watakiwa kukomboa bomba la mafuta

Bomba kubwa la mafuta nchini Marekani limeripotiwa kuwalipa wahalifu wa mtandaoni wanaofahamika kama DarkSide kiasi cha dola milioni tano $5m (£3.6m) kama kikombozi ,baada ya bomba hilo kuvamiwa mtandaoni.

Bomba la Colonial lilikuwa linapata wakati mgumu kufanya shughuli zake baada ya kudukuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha kuzimwa kwa huduma za mtandaoni katika bomba hilo kwa muda wa siku tano na hivyo kufanya usambazaji wa mafuta kuwa mgumu katika maeneo yote Marekani.

Ripoti kutoka CNN, the New York Times, Bloomberg na the Wall Street Journal all zinasema kikombozi kililipwa kwa kunukuu vyanzo vyake.

BBC imewasiliana na Colonial kwa maelezo.

Siku ya Ijumaa, wateja wa teknolojia kubwa ya Japan ya Toshiba walisema upande wa ulaya nchini Ufaransa ulikuwa umeshambuliwa na genge hilo hilo la wahalifu wa mtandaoni .

Colonial imetangaza kurudisha operesheni zake siku ya Jumatano lakini ilitoa angalizo kuwa itachukua siku kadhaa kuanza kusambaza bidhaa na kurudi katika taratibu zake za kawaida.

Usitishwaji wa usamazaji wa mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya ndege katika taifa zima la Marekani kumesababisha bei za bidhaa hizo kupanda na sheria ya dharura kupitishwa Jumatatu ya kutangaza hali ya dharura.

Bomba hilo kwa kina la Colonial linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku – sawa na 45% ya mahitaji ya mafuta ya Pwani ya Mashariki nchi hiyo na liinasambaza mafuta ya dizeli, ya petroli na mafuta ya ndege.

bomba

Wahalifu wa mtandaoni walifanya hujuma dhidi ya bomba ambalo limeshindwa kushindwa kufanya kazi tangu siku ya Ijumaa na mpaka sasa bado oparesheni ya kujaribu kurudisha huduma za bomba hilo zinaendelea.

Hali ya dharura inaruhusu mafuta kusafirishwa kwa njia ya barabara.

Jumla ya majimbo 18 yamepewa muda kidogo kusafirisha mafuta ya petroli, dizeli, ya ndege na aina nyingine za bidhaa za mafuta.

Majimbo hayo ni Alabama, Arkansas, Columbia, Delaware, Florida, Georgia, Kentucky, Louisiana, Maryland, Mississippi, New Jersey, New York, North Carolina, Pennsylvania, South Carolina, Tennessee, Texas na Virginia.

Bomba hilo la Colonial linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku

Jumapili jioni ilisema licha ya kuwa njia nne kuu zimezimwa, kuna njia nyingine ndogo kutoka eneo moja mpaka sehemu ya kupokelea mizigo ambayo inafanya kazi.

“Mara tu baada ya kubaini shambulio hilo, Colonial iliamua kuzima mifumo mingine kama tahadhari la tishio.

Hatua hii iliathiri kwa muda utendaji wa bomba hilo na kuathiri mfumo wa taarifa ambao ulikuwa unarudisha huduma,” kampuni hiyo imeeleza.

Wadukuzi hao waliacha maandishi kama hayo kwenye komputa walizofanya udukuzi

Wakati wadukuzi hao wa DarkSide sio genge kubwa katika eneo hilo lakini tukio hilo linaongeza hatari ya kuathiri miundombinu ya taifa viwanda na sio biashara peke yake.

Vilevile inaashiria kuongezeka kwa mfumo wa uhalifu wa kihalifu katika mfumo wa teknolojia ambao una thamani ya mamilioni ya pauni, ambayo ni tofauti na kitu chochote ambacho sekta viwanda ya usalama wa mtandao imewahi kukukabiliana nayo.

Ukiachana na ilani iliyoachwa kwenye komputa , waathirika wa shambulio la DarkSide walipokea kifurushi cha habari kuwajulisha kuwa kompyuta na mifumo yao imedukuliwa.

Genge hilo liliorodhesha aina zote za data ambazo waliiba na kuwatumia waathirika kurasa binafsi ambayo ilivujishwa ambapo tayari data ilikuwa inachukuliwa na kusubiri kujichapisha yenyewe,hivyo kampuni inapaswa kulipa kabla ya muda waliopewa kufika.

DarkSide waliwaambia waathirika pia kuwa watatoa ushahidi wa data ambazo wako nazo na wanajiandaa kufuta zote katika mtandao wa wahanga wao.

Kwa mujibu wa Digital Shadows, kampuni ya usalama wa mtandaoni iliyopo inafuatilia wadukuzi wa mtandao ili kusaidia makampuni kutodukuliwa mtandaoni , DarkSide inafanya kazi kama biashara.

Genge hilo linafanya kazi kwa kuwa na mfumo ambao unaiba data ambayo inawashirikisha washirika kwa kutuma barua pepe ya kutaka jambo na namna ya kufanya shambulio.

Washirika wa genge la wadukuzi wa mtandaoni wanawalipa DarkSide asilimia kadhaa ya kile ambacho watakipata kwa shambulio lolote ambalo litafanikiwa.

Na kuachiwa kwa mfumo mpya mwezi Machi inaweza kuhifadhi data haraka zaii kabla ya genge la wahalifu alijatoa taarifa kwa vyombo vya habari au kuwaalika wageni kwa ajili ya mahojiano.

Bomba hilo la Colonial linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku

Jinsi gani wadukuzi waliweza ‘kuteka’ bomba la mafuta?

Kwa watu wengi, picha ya kiwanda cha mafuta inayowajia kichwani ni ya mabomba, pampu na vifaa vingine vikuukuu viliyopiga weusi kwa uchafu wa mafuta.

Ukweli ni kuwa bomba la Colonial linafanya kazi kwa njia ya kidigitali.

Mabomba na vifaa vyote vinavyotumika kuangalia na kudhibiti usambazaji wa mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya ndege katika mamia ya maili vinafanya kazi kidijitali.

Colonial inatumia teknolojia ya kiwango cha juu kuendesha operesheni za bomba hilo.

Operesheni zote za teknolojia hii zimeunganishwa na mfumo mmoja.

Na wataalamu wa masuala ya mtandao kama kama Jon Niccolls kutoka taasisi ya CheckPoint, anaeleza kuwa popote pale kwenye kuunganisha mfumo kuna hatari ya uvamizi wa kimtandao:

“Vifaa vyote ambavyo vinatumika kuliendelesha bomba hili la kisasa vinatumia kompyuta badala ya kudhibitiwa na watu,” alisema.

“Kama vifaa hivyo vimeunganishwa kupitia mtandao wa ndani wa kampuni na ukadukuliwa, basi bomba lenyewe linakuwa limeathirika katika shambulio baya la kimtandao.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents