Habari

Ofisi ya Waziri Mkuu yasherehekea Idd na wanafunzi wenye ulemavu

Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa chakula cha mchana na kushiriki pamoja na wanafunziwa Chuo cha Ufundi Stadi Yombo ambacho ni maalum kwa watu wenye ulemavu katika kusherekea sikukuu ya Idd El Fitr.

Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Yombo ambacho ni maalum kwa watu wenye ulemavu, wakiwasikiliza viongozi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambao walikwenda chuoni hapo kwa lengo la kula nao chakula cha mchana katika kusherekea sikukuu ya Idd El Fitr

Akimwakilisha Waziri Mkuu katika tukio hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Ummy Nderiananga, amesema lengo la kuandaa chakula hicho ni kuendeleza umoja na kutoa faraja kwa kundi hilo la watu wenye ulemavu.

Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira naWenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu, akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Yombo ambacho ni maalum kwa watu wenye ulemavu.

“Katika kusherekea sikukuu hii ya Idd El Fitir, Ofisi ya Waziri Mkuu iliona ni muhimu kuandaa chakula cha mchana na kushiriki pamoja na vijana wetu wa chuo hiki cha watu wenye ulemavu hivyo Waziri Mkuu pamoja na Waziri wetu wa Nchi, Mhe. Jenista Mhagama wamenituma niwawakilishe katika tukio hili kwasababu wao wapo katika
majukumu mengine ya kitaifa,” amesema Ummy Nderiananga.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye Ulemavu), UmmyNderiananga, akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Yombo, alipotembelea chuo hicho kwa ajili ya kushiriki chakula cha mchana na wanachuo hao katika kusherekea sikukuu ya Idd El Fitr.

Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo, Prof. Jamal Katundu, ametoa wito kwa taasisi na watu binafsi kujenga utamaduni wa kuyajali na kuyasaidia makundi mbali mbali ya watu wenye mahitaji maalum kikiwemo chuo hicho cha watu wenye ulemavu.

Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Yombo ambacho ni maalum kwa watu wenyeulemavu, wakishiriki chakula cha mchana na viongozi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuuambao walitembelea chuo hicho katika kusherekea sikukuu ya Idd El Fitr.

“Hili jambo kubwa sana na ndio maana mimi kama Naibu Katibu Mkuu nimepewa jukuma la kuratibu suala hili na kama mlivyoona vijana wetu wamefurahishwa sana na tukio hili hivyo natumie fursa hii kutoa wito kwa watu wenye uwezo na taasisi mbali mbali zenye mafungu ya kusaidia jamii kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuja kuwasaidia vijana wetu,” Prof. Jamal Katundu.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa mkono wa Idd kwa baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Ufundi Stadi Yombo, alipoambataana na viongozi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kwenda kushiriki chakula cha mchana na wanachuo hao katika kusherekea sikukuu ya Idd El Fitr.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Mariam Chelangwa, amesema menejimenti pamoja na wanachuo wamelipokea tukio hilo kwa furaha sana ambapo ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa tukio hilo.

Aidha, baadhi ya wanachuo wakiwemo Joseph Baraza na Evodia Mwombeki wameelezwa kufurahishwa na tukio hilo na wameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na viongozi mbali mbali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambao walijumuika nao katika chakula hicho.

“Tumefurahi sana kwa namna moja ama nyingine kwasababu huwa tunajisikia furaha sana kujumuika na watu tofauti tofauti na kujiona kwambahatujatengwa…tunawashukuru sana kwa tukio hili la leo na Mungu awabariki sana,” amesema Evodia Mwombeki, Mwanafunzi katika fani ya Kilimo na Ufugaji.

Chuo cha Ufundi Stadi Yombo cha watu wenye ulemavu ambacho kipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kilianzishwa mwaka 1973 kwa malengo ya kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana wenye ulemavu nchini. Kwasasa kina jumla ya wanafunzi 76 na kinatoa kozi mbali mbali zikiwemo; Ufundi Umeme, Uwashi, Ushonaji, Uchomeleaji Vyuma pamoja
na Kilimo na Ufugaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents