Habari

MWANZA: NGO’s zapigwa marufuku kugawa kondomu na vipandikizi mashuleni

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mery Tesha ametoa onyo kwa taasisi zisizo za Serikali kuacha kuwaweka vipandikizi wanafunzi wa kike na kugawa kondomu mashuleni kwani wanahamasisha ngono kwa umri mdogo.

Mery Tesha

 

Mhe. Tesha ametoa kauli hiyo leo Machi 6, 2018 wakati wa maonyesho ya siku mbili ya wanawake katika viwanja vya Ghandh All jijini Mwanza.

“Wanafunzi hawa tuwalee katika maadili mema yanayostahili badala ya kuwapatia kondomu na vitu vingine vinavyohamasisha kufanya ngono, jambo hili halikubaliki hata kidogo,” amesema Tesha.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa baraza la watoto Mkoa wa Mwanza, Neema Theonest amesema katika Tanzania ya viwanda ya kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ni vyema kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake vijijini.

Neema amewataka wanawake wote nchini waache kubweteka badala yake wajitume kufanya kazi ili kupandisha uchumi kuanzia ngazi ya familia na kutokomeza umasikini.

Chanzo:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents