Burudani

Rais Kenyatta awapongeza waigizaji wa filamu ya ‘Watu Wote’

Filamu ya ‘ Watu Wote’ inayohusu shambulizi la kigaidi la al-Shabab nchini Kenya ambayo lilitokea mwaka 2014 haijafanikiwa kushinda tuzo ya Oscar.

Licha ya kukosa kushinda, Wakenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wamekuwa wakiwapongeza walioshiriki walioigiza katika filamu hiyo kwa kuwasifu wamefanya kazi. Rais Kenyatta ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwapongeza waigizaji hao.

https://twitter.com/PresidentKE/status/970597534635872261

‘Watu Wote’ ilikuwa ikisifiwa na ilikuwa ikielezea tukio la uhalisia  kwa kifupi hakikuweza kushinda na badala yake  filamu ya ‘The Silent Child’ iliyoigizwa na  Rachel Shenton na Chris Overton wanatokea Uingereza waliweza kunyakuwa tuzo hiyo katika kipengere cha ‘Filamu Fupi kuhusu Matukio Halisi’.

Filamu ya ‘The Silent Child’ ilitoka mwaka 2017 ambapo  inaelezea maisha ya msichana wa miaka minne asiyeweza kusikia anayeishi maeneo ya mashambani Uingereza. Huku filamu ya ‘Watu Wote/All of Us’ inazungumzia shambulizi la kigaidi la Al-shabaab lililotokea nchini Kenya mwaka 2014 katika eneo la Mandera ambapo watu 28 waliuawa kwenye tukio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents