FahamuHabari

Mwijaku kumlipa Maua Sama milioni 300 au aende Mahakamani

Baada ya Mwijaku kusema na kuandika maneno ya udhalilishaji kwa Msanii Maua Sama.

 

Maua Sama Kupitia Wakili wake Claudio Msando kutoka kampuni ya Mawakili na Wanasheria ya Msando Law Office iliyopo Jijini Dar es Salaam – Tanzania, wamemuandikia Mwijaku hati ya madai na kumpa Masaa 24 ya kujibu tuhuma hizo za udhalilishaji ikiwa ni pamoja na fidia ya Fedha za Kitanzania Shillingi Milioni Mia Tatu.

Endapo atashindwa kufanya hivyo, basi atapelekwa Mahakamani na hatua nyingine za Kisheria zitafuata.

Siku ya Tukio la miaka 20 ya Alikiba Mwijaku aliongea na Wana habari na moja ya maneno ya udhalilishaji aliyoyatamka kwa Maua Sama ni kwamba:-

“Maua Sama ana kaumalaya fulani anataka kumharibia Alikiba, ndio maana haolewa mwanamke gani haishi na Mwanaume ameishi na Wazungu na wazee wamemkibia”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents