Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariUmbea

Mwijaku: Ommy Dimpoz tusameheane, Usijipe laana, usihuzunike wala usilie

Kupitia Instagram yake Mwijaku ameandika kuwa: #TUSAMEHEANE-Kabla maharagwe hayajapikwa, huchambuliwa kwanza, ambapo yale maharage yalo mabovu hutupiliwa mbali ili yale mazuri yaweze kupikwa.

Hata hivyo, mvua inapokuja, yale maharage mabovu yaliyotupwa ardhini hugeuka kuwa mbegu, humea, ikakua na kuchanua kuwa maharage mazuri tena.

Na yule aliyeyajaji kuwa ni mabaya na kuyatupa huenda yatakapokomaa akavuna na kuyala kwa afya.

Kupitia #OmmyDimpozi nimejifunza Na maisha ndivyo yalivyo, unaweza ukatengwa, ukasemwa, ukadharauliwa na kuumizwa vibaya na wale uliowaamini. Lakini, Je, ni nani ajuaye njia za Mwenyezi Mungu?

Hao hao waliokuumiza itatokea siku watakutazama wakitegemea la kheri kutoka kwako. Huenda wakakupigia magoti kabisa wakihitaji walau neno lako moja tu wapone!

Usijipe laana, usihuzunike wala usilie pale Dunia inapokuegemea. Ni suala la muda tu kupata Mvua yako ya baraka! Mazungumzo yangu na mzee nyembo haya kua na lengo la kuharibu image yako hata mara moja . Najua story vizuri nia yangu ni kumpa furaha mzee tu .

Kupia video yako nikwambie tu ,Your germination moment is just around the corner! Pray, Believe, and Receive!! God bless y’all.

Love you my broo .! Let us forgive each other . Innah Llah Maaswabireen .Love You Broo 🙏🏾

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents