HabariSiasa

Utapanga foleni ya zaidi ya masaa 30 kuuaga mwili wa Malkia Elizabeth II

Waziri wa utamaduni wa Uingereza Michelle Donelan ameonya kuwa huenda kukawa na misururu mirefu kuliko inavyotarajiwa kuufikia mwili wa Malkia Elizabeth II katika ukumbi wa Great Hall wa Westminster.

Alisema kuwa huenda kukawa na mistari mirefu ya maelfu ya wafariji, na unaweza kusubiri kwa saa 30 mstarini kabla ya kufika Great Hall.

Kwa misingi hii, aliionya jamii kujianda kusimama saa nyingi kila siku, na kujiandaa kuihimili hali ya hewa.

Lakini alisema, “Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha watu waliosafiri kuja London hawana matatizo yoyote.”

Bi Donelan alisema kwamba zaidi ya watu 1,000 watakuwa wakisubiri kwenye mstari kila siku kuwasaidia.

Aliongeza kuwa Tate Modern na Shakespeare Globe watawasha mataa kwenye ofisi zao mjini London pamoja na kuweka picha ya Malkia Elizabeth, na maduka yatasambaza viburudisho kwa umma.

Vyumba 500 zaidi vimehifadhiwa kwenye barabara inayoelekea katika ukumbi wa Westminster kukidhi mahitaji ya umma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents