Burudani

Nahreel aanza kuandikisha wanafunzi wa chuo chake cha muziki ‘Tims’

Producer Nahreel amedhamiria kutoa mchango wake katika sanaa ya muziki wa Tanzania, kwa kuamua kuanzisha chuo cha muziki ili kushare uzoefu na ujuzi wake kama msanii na producer kwa vijana wengine ambao wana ndoto za kufanikiwa katika fani hiyo.

Nahreel

Baada ya kutangaza kuanzisha chuo cha muziki hivi karibuni, The Industry Music School (TIMS), sasa ameanza kupokea wanafunzi. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Nahreel ameandika kuwa wameanza kuandikisha wanafunzi wapya ambao kwa muhula huu wa kwanza watachukua wanafunzi 30 tu.

Siku za karibuni producer huyo alisema baadhi ya waalimu watakaoungana nae katika kutoa elimu na ujuzi kwa wanafunzi wa TIMS ni wasanii wenzake wa Good Music Family, wakiwemo Nikki Wa Pili wa Weusi, Aika wa Navy Kenzo na Vanessa Mdee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents