Burudani

Nahreel kufungua chuo cha muziki ‘TIMS’

Producer Nahreel na msanii wa kundi la Navy Kenzo, anaanzisha chuo cha muziki chini ya studio yake ya The Industry.

Tims

Nahreel amesema kuwa mafunzo yatakayotolewa katika chuo cha TIMS (The Industry Music School) ni pamoja na utengenezaji wa midundo, ufanyaji wa mixing na mastering, kutunga, kurap, kuimba,na usimamizi wa biashara ya muziki.

“Classes zitaamza karibuni tu..tutakuwa tunauwezo wa kuchukua wanafunzi wengi tu na kuwafundisha kwahiyo haya madarasa yataanza soon tu na tutatoa taarifa.” Ameiambia 255 ya XXL.

Nahreel

Nahreel ameongeza kuwa wanafunzi watakaopata nafasi ya kuchukuliwa na TIMS ni wale tu wenye uwezo wa kufanya muziki.

“Kwanza hatutakubali kuanza kuchukua mwanafunzi yoyote tu, tutaanza kuzingatia kwanza mwanafunzi lazima kidogo awe na uelewa wa muziki kidogo hata kama hajawahi kufanya muziki basi awe anaupenda muziki, kwahiyo tutafanya audition ili tuepuke usumbufu wa kufundisha tu watu fulani ambao hawataweza kufanya vitu ambavyo tunafundisha…Shule itakuwa ni miezi mitatu kwa kozi moja, na nimpango wa kuwa na wanafunzi 30 mpaka 40 kwa hiyo semester.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents