Burudani

Nahreel aitaja siri ya mafanikio ya Navy Kenzo

Ili msanii aweze kufanya kazi nzuri anahitaji kuwa na timu nzuri na iliyokamilika kwenye kila idara.

navy

Ndio maana kundi la Navy Kenzo linaloundwa na couple ya producer Nahreel na Aika wamegundua hitaji la kuwa na timu, na huenda ndio sababu kuna mabadiliko makubwa katika show zao, video zao na muziki wao kwa ujumla kwasababu hivi sasa wanafanya kazi na timu kubwa.

Nahreel amesema kuwa wameamua kuunda timu ya watu sita wanaoshughulikia mambo tofauti wakiwemo mameneja wawili, designer, mtu wa makeup, mpiga picha pamoja na page manager.

“Sasa hivi tuna timu kubwa ambayo tofauti na kama tulivyokuwa tunafanya kazi zamani,” alisema Nahreel kupitia 255 ya XXL.

“tunawatu kama sita, tuna mameneja wawili, mmoja anasimamia upande wa marketing lakini kama meneja wetu pia, tuna meneja wetu ambaye anatembea na sisi kila siku, tuna page manager tuna mpiga picha, designer, makeup…” alisema Nahreel.

Producer huyo aliongeza “nadhani tumerisk, sio kurisk lakini ndio vitu vinavyotakiwa vifanyike hivyo, ukijumlisha na sisi tupo kama watu nane, ambapo hapo hamna madancer au nini yaani hao ni watu tu ambao wako kwenye management.”

Baada ya ‘Game’ inayofanya vizuri kwasasa, Nahreel amesema kuna video nyingine na collabo ya kimataifa inakuja pamoja na album.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents