Burudani

Nash MC alia na rappers waliowahi kushinda tuzo, asema hawaitetei hip hop

Rapper Nash MC amedai kuwa wasanii wote wa Hip Hop nchini waliowahi kushinda tuzo mbalimbali ama wenye nafasi kwenye jamii hajawahi kufanya kitu chochote kuutetea muziki huo.

Nash-492x350

Akizungumza Jumamosi iliyopita kwenye kipindi cha X Ray cha EFM, Nash alisema wasanii hao hakuna walichofanya ilhali wakishuhudia muziki wa Hip Hop ukididimizwa kwa kauli za kuwakatisha watu tamaa kuhusu muziki huo.

“Nisingependa kuzungumzia mambo yangu binafsi kwa sababu kuna matatizo yametokea, matatizo haya yanahusu utamaduni mzima wa Hip Hop. Mimi ningeomba kuna masuala yamekuwa yanachanganya sana, miaka ya hivi karibuni watu wamekuwa wakiizungumzia Hip Hop vibaya sana. Hip Hop imekuwa ikizungumziwa vibaya na kinachonisikitisha zaidi wasanii wote waliopewa dhamana ya Hip Hop kwa maana kwamba waliowahi kupewa tuzo mwanzoni mpaka sasa hakuna walichofanya kukaa na kuongelea na kuitetea Hip Hop,” alisema Nash.

“Sio waliopewa tuzo mwanzo wakati zinaanzishwa mpaka huyu aliyepewa juzi, wote waliopewa tuzo ambazo zinaitwa ni Hip Hop hawajafanya kitu chochote kwenye kutetea Hip Hop na kwaajili ya watu wa Hip Hop na kwa jamii nzima ya Hip Hop. Sasa ivi kuna jambo kubwa linaendelea, hili suala la Hip Hop sio muziki wa biashara, Hip Hop sijui ni ugumu, huu mtazamo anauleta nani? Huu mtazamo kwanini unapendwa? Kuna baadhi ya watangazaji, baadhi ya radio, baadhi ya watu wanaipotosha jamii,” aliongeza.

“Nikupe tu neno dogo sana niwape faida watanzania, utamaduni wa Hip Hop kazi yake ni kusambaza Love, Peace, Unity and Happiness ndio Hip Hop kitu ambacho tunasambaza na tuna kanuni zetu zinakataza yale yote yaliyokuwa mabaya. Lakini leo hii radio baadhi ya watangazaji walioajiriwa kupitia kaka zao ama ndugu zao, hizi kazi za kuitwa radioni ‘njoo nishamwambia kaka yako kesho utaingia utatangaza’, watangazaji wa namna hii ndio leo hii wanatuaribia utamaduni wa Hip Hop. Mimi nawaomba kama haujui Hip Hop au haufatilii Hip Hop achana na kuiongelea Hip Hop vibaya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents