Burudani

Nay wa Mitego kuachia wimbo mpya ‘nina jambo kubwa kwa ajili yako soon’

Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego wakati akiendelea kufanya vizuri na wimbo ‘Sijiwezi’ ametishia kuachia kazi mpya hivi karibuni.

Rapper huyo ambaye ameonyesha mabadiliko makubwa ya uimbaji katika wimbo ‘Sijiwezi’, hivi karibuni aliiambia Bongo5 bado ndani ana ngoma zakutosha ambazo anaweza kuziachia muda wowote.

Alhamisi hii rapa huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wake mpya.

“MrPretender???? Anza ku Subscribe kwenye YouTube Chanel Yangu #MrNay Nina jambo Kubwa kwa ajili yako soon. Go and Subscribe to my YouTube Chanel #MrNay i got something big for you. Soon.,” aliandika rapper huyo kupitia instagram.

Nay ni mmoja kati ya wasanii wa hip hip ambao wanafanya vizuri katika muziki wao kwa muda mrefu bila kutetereka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents