Burudani

Ndugu wa Q Chief wataka mtoto wao anunuliwe nyumba, gari ya tsh milioni 35 kama alivyoahidiwa na QS Mhonda

Familia ya msanii wa muziki Q Chief wamemtaka meneja wa msanii huyo QS Mhonda kurekebisha mkataba wa mtoto wao huku ndani ya mkataba huo wakitaka msanii huyo kununuliwa nyumba, gari ya tsh milioni 35 pamoja na bima ya maisha kama alivyoahidiwa katika mkataba wake uliyopita.

Wakizungumza katika kipindi cha Enewz cha EATV, wazazi hao wamedai wameamua kuingilia kati mkataba wa msanii huyo na kusema mkataba huo unamfanya mtoto wao aishi maisha magumu kiasi cha kushindwa kuchangia mambo yakifamilia.

“Hapa tumetaja vitu ambavyo alitakiwa kumpatia kijana wetu, moja ni kumpatia nyumba ambayo ataimiliki yeye mwenyewe ambayo inaweza ikawa na vyumba vitatu lakini yakisasa ndani ya miaka miwili katika mtakaba wake, pili awe na bima ya maisha ambayo itamsaidia yeye pamoja na watu wake wa nne, tatu aweze kumiliki gari la kisasa kama ambayo wanatembelea wasanii wengine, kuliko maisha ambayo anayapitia kwa sasa anapitia katika maisha magumu sana, hana usafiri na sisi tulikuwa tumepropose apatiwe gari isiyopungua ya tsh milioni 35 lakini mpaka sasa hivi kijana wetu tumeona anapata matatizo hata kuudhuria katika mambo ya kifamilia anashindwa

Pia alisema familia hiyo imeamua kumuandikia barua bosi wa Q Chief ambaye ni QS Mhonda kumuomba kubadilisha sehemu mbalimbali ambazo zinambana sana kijana wao kiasi cha kumsababishia kurudi alipotoka jambo linaloweza kumvurugia maisha yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents