Burudani

Sakata la Unga: TID, Recho, Tunda waachiwa kwa dhamana, Wema abaki

Watuhumiwa wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamm, Paul Makonda, Jumanne hii, February 7, 2017 wamefikishwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazowakabili.

Lulu Diva

Mastaa hao wakiwemo TID, Nyandu Tozi, Babu wa Kitaa, Romy Jones, Tunda, na wengine, wameachiwa kwa sharti la dhamana ya shilingi milioni 10 kila mmoja na watakuwa wakiripoti kwa mwezi mara mbili huku wakiwa katika uangalizi wa jeshi la polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Ni furaha tu lakini: Tunda akimnong’oneza kitu Recho wakati wa kesi yao Jumanne hii kwenye mahakama ya Kisutu. Wengine ni Nyandu Tozi, TID, Director Joan, Romy Jones na Mchaff Chakoma

Hata hivyo watuhumiwa wengine wakiwemo Petit Man, Said Alteza, Lulu Diva na wengine wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20 na watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa hao watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.

It’s all good

Hali imekuwa tofauti kwa Wema Sepetu ambaye ameendelea kukaa rumande baada ya msako kubaini msokoto wa bangi nyumbani kwake na hivyo kuongezwa kosa jingine zaidi ya lile la awali, ambapo sasa inasubiriwa uchunguzi kukamilika.

 

Petit Man (Katikati) akifuatilia kesi
Washukiwa wa sakata la madawa wakirudishwa polisi central baada ya kesi yao kusomwa mahakamani Kisutu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents