Habari

Mbeya: Mwanafunzi wa sekondari akamatwa akiuza dawa za kulevya

Wakati vita dhidi ya madawa ya kulevya ikiendelea Dar, imetua pia jijini Mbeya baada ya polisi kutangaza kumkamata mwanafunzi anayesoma sekondari akiwa na kete za cocaine eneo la Mbalizi jijini humo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Dhahir Kidavashari amesema kuwa polisi wamemkamata kijana huyo akiwa anaziuza dawa hizo kwa watu mbalimbali huku akisema upelelezi wa kuwadaka mapapa unaendelea.

Amesema vita dhidi ya madawa ya kulevya imepata msukumo mpya ambao unalenga kuukata mnyororo mzima wa mtandao unaosambaza dawa hizo.

Mapema Jumatatu hii Rais Magufuli alimuunga mkono Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na jitihada zake dhidi ya biashara hiyo haramu huku akiagiza jeshi la polisi kuwashughulikia wale wote wanaojihusisha na madawa ya kulevya bila kujali wadhifa wao.

By: Emmy Mwaipopo

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents