Burudani

Nikki wa Pili ajibu ngoma nyingi za hip hop Bongo kukosa verse 3 kama awali (+video)

Msanii wa muziki Bongo, Nikki wa Pili amefunguka kutoweka kwa utamaduni wa ngoma nyingi za hip hop kuwa na verse tatu.

Rapper huyo kutoka kundi la Weusi amesema muziki unaendana na mapokeo yake na media nyingi sasa zinapiga muziki verse moja au mbili, pia wasanii wa Bongo Flava hawataki kukumbwa na kitu kilichokumba muziki wa band au taarab kutoka na nyimbo zao kuwa refu.

“Kwa hiyo watu wa media sasa hivi time zao ni ndogo, wanahitaji nyimbo fupi ili waweze kupiga muziki mwingi ili mtu anayesikiliza aone muziki unaenda ukibadilika, kwa hiyo sisi kama wasanii wa kizazi kipya tumeenda na time,” Nikki ameiambia Bongo5.

“Ukisema sasa unapiga verse tatu hamna mtu atasikiliza na kama unapiga inabidi iwe fupi, ndio maana ukisilikiza wimbo kama Dude au Madaraka ya Kulevya verse yangu ina mistari kama nane au 12 tu” ameongeza.

Nikki kupitia kundi la Weusi kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma yao mpya ‘NiCome’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents