Habari

Video: Rais Magufuli ataka wanaosema vyuma vimekaza wapelekwe mahakamani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wanaotoa takwimu za uongo kwa kuzipika kukamatwa na kupelekwa mahakamani ili wakitoka huko wajifunze.

Rais Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma, ambapo pamoja na hayo amesema kuwa ukikosea kutoa takwimu umeichafua nchi.

“Hata mtu akija na takwimu za kupikwa kwamba vyuma vimekaza, mpelekeni Mahakamani akaeleze ametoa wapi hizo takwimu. Ninaomba kurudia tena, Watanzania tujifunze kuheshimu takwimu,” amesema Rais Magufuli.

“Ukikosea kutoa takwimu umeichafua nchi, takwimu ni kitu kibaya sana ndiyo maana kuna watu wamebobea kwenye takwimu hivyo wananchi tuwasikilize watu wa takwimu asitokee mtu mwingine akatoa takwimu tofauti na zile walizonazo watu wa takwimu. Mtu anasema vyuma vimekaza wakati watu wa takwimu wanasema vyuma vimefunguka watu hawa wanatakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani ili wakajifunze kutoa takwimu huko,” alisema Rais Magufuli

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents