Burudani

Nimejaribu kuacha muziki nimeshindwa – Lord Eyes

Msanii wa hip hop Bongo, Lord Eyes amefunguka kuhusu kuacha muziki na kufanya mambo mengine.

Rapper huyo ameiambia Funiko Base ya Radio Five kuwa hana mpango wa kuacha muziki kwa sasa ila ni kitu ambacho amewahi kujaribu.

“Nina albamu mbili halafu hata moja haikwenda sokoni lakini bado narekodi, sichoki kurekodi am keeping recording ndio maana nawahaidi watu Load Eyes hawezi kuacha muziki,” amesema.

“Hata mimi nimejaribu kuacha muziki nimeshindwa kwa sababu muziki ni maisha yangu hata nikitaka kuacha nashindwa kwa sababu watu wananisumbua kuhusu muziki,” amesisitiza.

Loard Eyes kwa sasa anatamba na ngoma ‘Hardcore’ ambayo wamefanya kundi la Nako 2 Nako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents