HabariMichezo

Nina 5% za kupanda Ulingoni, epuka matapeli- Mwakinyo

Bondia Staa na mwenye mkwanja zaidi Nchini @hassanmwakinyojr baada ya hapo jana kuandika kuwa Hatopanda Ulingoni kutokana na uongo na udanganyifu wa Mapromota, asubuhi ya leo siku ya Ijumaa ameendelea na msimamo wake ule ule huku akiweka wazi ana 5% pekee.

“Maswali na simu zimekuwa nyingi, kiukweli mpaka sasa nina asilimia 5% Tu za kupanda ulingoni ikiwa zitaongezeka ni mimi mwenyewe nitasema naomba tuwe wavumilivu epuka matapeli…msimamo ni mmoja tu kama mogadishu.. kwa kitendo hichi naomba!! huu ndio uwe mwisho wa mapromoter dhulma wahuni wadanganyifu na matapeli…🙏,”- Ameandika Hassan Mwakinyo

Kumbuka pambano hilo limepangwa kuchezwa leo usiku lakini mpaka sasa Bondia Hassan Mwakinyo ameweka wazi msimamo wake kwa kile anachosema ni uongo na udanganyifu wa Mapromota

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents