Burudani
‘Nina maadui wengi’, asema Davido
Staa wa Nigeria, Davido anaamini kuwa ana maadui tena maadui wengi ambao wanajaribu kumshusha kutoka kwenye mafanikio aliyonayo.
Kupitia Twitter Davido ameandika “I got enemies, I got a lotta enemies Got a lotta people tryna drain me of my energy.”
I got enemies, I got a lotta enemies
Got a lotta people tryna drain me of my energy !!
— Davido (@iam_Davido) February 17, 2015
Hii si mara ya kwanza kwa Davido kulalamika kupitia Twitter juu ya watu ambao hawamtakii kheri, au aliowasaidia na baadae kusahau. Hata hivyo hajamtaja mtu yeyote hivyo haijulikani maadui anaowataja ni kina nani.
Davido anatarajiwa kutumbuiza nchini Kenya March 28.