Burudani

Nisher asema bei mpya anayotoza kushoot video ndio inayowakimbiza wasanii wengi

Mwishoni mwa mwaka 2013 muongozaji wa video nchini, Nisher alikuwa akitoza shilingi milioni 3 kushoot video moja ya muziki, na aliahidi kuongeza bei hadi kufikia dola 4000 pale vifaa vipya alivyoagiza vitakapowasili.

Nisher7

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Nisher amesema kwa sasa anatoza shilingi milioni 10 kwa video moja, ambayo inahusisha gharama zote za utegenezaji kama location, models, malipo ya director pamoja na usambazaji.

“Kwasasa video kwangu ni 10 million (production/director’s fee/ distribution), wasanii watatu nilio fanya nao kazi this year ndio pekee walio weza kunilipa hiyo hela! Wengine walipotea.” Alisema Nisher.

nisher location

Ameongeza kuwa bei hiyo ni moja ya sababu zilizomfanya mwaka huu kufanya video chache kutokana na wengi waliompigia kutaka kufanya kazi kutorudi tena baada ya kuwatajia pesa hiyo.

“Kuna baadhi ya wasanii wananicheki kufanya kazi za video ila changamoto kwao inakuja kwenye swala la hela, wakati wamalipo wanapotea, sita taja majina ila niwasanii wakubwa tu!” alisema Nisher.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents