Habari

Nmb yakabidhi msaada wa madawati 50 Hanang

Shule zilizopokea Misaada inayotolewa na benki ya NMB zimetakiwa kufanya vizuri katika masomo yao ili
kuonyesha thamani ya misaada hiyo. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Hanang,Ghibu  Ringo wakati
alipokuwa akizungumza baada ya kupokea msaada wa viti na meza  50 kwa ajili Shule ya Sekondari ya Getwanasi
iliyopo wilayani hapa .

Mkuu wa Wilaya ya Hanang ,Ghaibu Ringo (wapili kulia ) akipokea msaada wa viti na meza 50 yenye thamani ya shilingi milioni tano kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kati ,Nsolo Mlozi (kushoto) kwaajilli ya Shule ya Sekondari Getwanasi wilayani Hanang. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang,Rose Kamili.

Ringo alizitaka shule zilizopokea msaada kutoka NMB kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo na mitihani yao
ili kuonyesha thamani ya mchango huo.

“Unajua hata kama una mtoto wako unamilipia ada vizuri na kumnunulia mahitaji muhimu unategemea kuona
matokeo yake mazuri,sasa hata ninyi shule hii  na wengine ambao wameshapokea misaada mbalimbali kutoka
NMB nataka kuona  mnaonyesha mafanikio zaidi katika masomo yenu”alisema.

Alisema lazima wanaopata misaada hiyo kutoka Nmb na wadau wengine wa elimu na maendeleo kuonyesha
thamani ya fedha zinazotolewa ili kuwatia moyo wa kuendelea kuwapa wengine.

“Haiwezekani mdau unakupa vifaa vizuri kama hivyo lakini matokeo anasiki shule hiyo imekuwa ya mwisho
anajisikia vibaya kwa sababu lengo lake ni kukusaidia ufanye vizuri katika masomo yako”alisema
Aidha aliwataka aliwataka wakuu wa shule na kamati za shule kuweka mikakati ya kuvitunza vifaa vinavyotolewa
na wadau wa maendeleo, Alisema misaada inapotoka inarekodiwa vizuri na uongozi wa halmashauri hivyo haiwezekani shuel hiyo hiyo kuendelea kuomba msaada wa vifaa hivyo  kila.


Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hanang,Solomon Shati alisema halmashauri hiyo inazo shule
sekondari 36  na kati ya shule hizo,  ya binafsi ni moja tu,
Shati alisema kuwa kati ya shule hizo za serikali benki ya Nmb imetoa misaada kwa shule mbili kwa mwaka jana na
mwaka huu ambapo msaada huo umesaidia kuleta mabadiliko kwa kuongezeka kwa kiwango ufaulu huko.
Kadhalika aliwashukuru NMB kwa misaada hiyo kwani imekuwa ikisaidia kupunguza mzigo kwa wanachi kwa
wazazi kwani walitakiwa kununua mahitaji hayo
Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Rose Kamili alisema misaada ya Nmb imekuwa ikilenga maeneo ya wananchi wa
uchumi wa chini jambo ambalo limekuwa likiigusa jamii.
Aliitaja misaada ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati pamoja na viti imekuwa chachu ya maendeleo ya
elimu na jamii nchini.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema msaada huo wa viti na meza 50 uliotolewa
na NMB unathamani ya milioni tano na unatokana gawio la faida iliyopata benki na kuirushia jamaii kutokan ana
kuwaunga mkono Mlozi alisema benki hiyo inatenga asilimia moja ya mapato yake kila mwaka na kuirudisha kwenye jamii kwa kutoa misaada katika sekta ya afya,elimu na majanga mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang ,Ghaibu Ringo (katikati) akiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kati ,Nsolo Mlozi (kushoto) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hanang,Rose Kamili wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa Shule ya Sekondari Getwanasi wilayani Hanang – Manyara.

Alibanisha kuwa kutokana na serikali kuwa hisa za asilimia 38 wameona kuunga mkono juhudi za zake katika kutoa
elimu kwa kuchangia vifaa   vya elimu na ujenzi wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi waliochaguliwa na
kushindwa kuanza masomo kutokana na upungufu wa vyumba kuanza masomo mwezi huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents