Rais Magufuli ‘Hakuna lisilowezekana kwa Mungu, tulishinda mwaka jana na tutashinda sasa’ (Video)

Rais John Pombe Magufuli ametangaza siku tatu za maombi ya kusali na kufunga na ili kuyashinda matatizo yanayolikabili taifa ikiwemo maradhi ya corona ambayo yanaisumbua dunia.

Rais Magifuli amesema hakuna lisilowezekana kwa Mungu “Mungu ndiye muweza wa yote ninashukuru viongozi wa wetu wa dini mmendelea kulihubiri hili, tuendelee ndugu zangu watanzania kusimama na Mungu tulishinda mwaka jana inawezekana hili ni jaribu lingine nalo tukisimama na Mungu tutashinda”.

Akiwaongoza waombolezaji waliofika kwenye viwanja vya Kareem jee kuaga mwili wa aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi amesema magonjwa yamekuweko na yataendelea kuweko na si kwa Tanzania pekee bali kote duniani na hivyo hakuna sababu ya kutishana bali watu wa sali na kuchukua tahadhari.

Aidha Rais Magufuli amethibitisha waziri wa fedha na mipango Dokta Philip Mpango yuko hai licha ya kwamba ni mgonjwa na anaendelea vyema na matibabu ,na kuwaonya wale wote wanao wazushia watu vifo wakiwemo viongozi kwani huo si uungwana wala ubinadamu.

Rais Magufuli pia ametoa pole kwa familia na watanzania kwa ujumla kwa msiba wa Maalim Seif Sharif Hamad,aliyekuwa Makamo wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na kusisitiza taifa limepoteza kiongozi imara mwenye upendo na aliyekuwa na moyo wa kusamehe .

Amesema Maalim Seif alimuandika barua ya kutaka kumuona mara tatu na mara mbili za awali alishauriwa asubiri kwanza lakini alipomuandikia mara ya tatu alimwita na alipokutana na kuzungumza naye aligundua alikuwa mtu wa tofauti na taswira iliyokuwa imejengeka kichwani mwake ambapo pia alimuhakikishia.

Rais aliyechaguliwa Zanzibar ataongoza kwa amani miaka yake mitano na hakutakuwa na fujo wala vurugu yoyote Mwishoni mwa mwezi Januari Maalim Seif Sharif Hamad alitangaza kuwa ameambukizwa maradhi ya Corona na tangu wakati huo hakuonekana tena hadharini mpaka mauti yalipomfika Februari 17, 2021.

Tangu kuanza kwa wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona duniani mamlaka nchini Tanzania hazijatoa taarifa ya wazi kueleza ikiwa nchi hiyo inatambua juu ya uwepo wa maradhi hayo nchini humo na hatua inazochukua kuwalinda raia wake licha ya kwamba kumekuwa na matamko tata juu ya swala hilo na wengi wa viongozi serikali wamekuwa wakihimiza raia kutumia njia za asili kujikinga ikiwemo kujifukiza na kunywa dawa zitokanazo na matunda na viungo mbali mbali.

Related Articles

Back to top button
Close